Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (hawapo pichani), akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma walio katika halmashauri hiyo.
………………………
Na. Veronica E. Mwafisi-Mufindi
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kuwajibikaji kikamilifu katika kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya na miundombinu ya barabara na reli, ili fedha inayotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza miradi hiyo itumike ipasavyo kuleta maendeleo katika taifa.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa watumishi wa umma nchini, alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutatua changamoto zinazowakabili na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa wilaya hiyo.
“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri zote nchini, hivyo ni lazima tuwajibike kikamilifu katika kuisimamia miradi yote ili ikamilike kwa wakati na kuwanufaisha wananchi,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kuwajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora ili kuondoa dhana potofu iliyojengeka katika jamii kuwa, watumishi wa umma hawawajibika ipasavyo kama ilivyo katika sekta binafsi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bw. Kenny Shilumba amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kuhimiza uwajibikaji, kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na kutatua kero na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili watumishi walio katika halmashauri yake.
Naye, Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bi. Tunu Kombo kwa niaba ya watumishi wenzie amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kuwapatia elimu kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutumishi, ikiwa ni pamoja na kutatua kero na changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.
Sanjari na hilo, Bi. Komba amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuteua viongozi mahiri wenye kujituma katika kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma nchini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameanza ziara ya kikazi mkoani Iringa kwa kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (hawapo pichani), akiwa katika ziara yake ya kikazi yenye lengo kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma walio katika halmashauri hiyo.
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa halmashauri hiyo.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Sigifridi Kaunara akitoa taarifa ya hali ya watumishi katika halmashauri ya wilaya hiyo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri hiyo.
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bw. Robert Semaganga akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi (wapili kutoka kushoto) akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Bw. Servi Ndumbaro.