Featured Michezo

YANGA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA SIMBA LIGI KUU YA NBC

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo,Mzalendo blogs

WAKIWA wenyeji wa Mchezo Mabingwa watetezi Yanga wameshindwa kutamba mbele ya Simba baada ya kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC iliyochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa watani wa Jadi uliosimamisha nchi kwa dakika 90 uliohudhuriwa na wadau wa mchezo mashabiki wa timu zote mbili uwanja wakipambwa na jezi za Njano,Kijana na Nyekundu na Nyeupe.

Simba walianza kupata bao kupitia kwa winga wao hatari  Augustine Okrah dakika ya 15 akimalizia pasi Clatous Chama huku Yanga wakipata bao kupitia kwa Kiungo Mshambuliaji wao Stephanie Aziz Ki dakika ya 45 baada ya kupiga Mpira wa faulo ulioenda moja kwa moja.

Kipindi cha Pili timu zote zilifanya mabadiliko huku kosakosa zikiendelea kila upande hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho hakuna aliyeweza kuondoka na pointi tatu.

Kwa matokeo hayo Simba wanaendelea kukaa kileleni wakiwa na Pointi 14 sawa na Yanga wenye Pointi hizo 14 huku Simba akifaidika na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

About the author

mzalendoeditor