Featured Kitaifa

BARRICK YALENGA UKUAJI ZAIDI NCHINI TANZANIA

Written by mzalendoeditor
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow akikabidhi mfano wa hundi ya dola 10,000 kwa Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Anger House Children’s Home, Holly Opondo (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika mkoani Mara . Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara,Bw.Yahya Nawanda
………………………….
Wakati migodi yake ya dhahabu ya North Mara na Bulyanhulu imejipanga kufikia uzalishaji wa pamoja wa zaidi ya wakia 500,000 kwa mwaka wa pili mfululizo, Barrick Gold Corporation, kwa msingi huu inatarajia kupanua shughuli zake Afrika Mashariki.
 
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika katika shule iliyopo karibu na Mgodi wa North Mara, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Bristow, alisema kufufuliwa kwa migodi hii ambayo ilikuwa imekufa na kubadilishwa kuwa raslimali yenye thamani kwa pamoja kujumuishwa katika hadhi ya daraja la kwanza (Tier One2) la uzalishaji ya migodi ya Barrick katika sehemu nyinginezo imekuwa hadithi ya mafanikio ya kushangaza.
 
“Msingi wa ushirikiano wetu na Twiga na Serikali ya Tanzania sio tu ulisuluhisha migogoro ya muda mrefu na waendeshaji wa awali wa migodi hii, lakini umeanzisha mfano wa ushirikiano unaoleta faida kati ya wachimbaji madini na nchi wenyeji, hususani barani Afrika. Kwa kudhihirisha kuwa Tanzania ni sehemu yenye mazingira rafiki ya uwekezaji pia kuweka mustakabali mzuri wa tasnia ya madini nchini katika siku zijazo,” alisema.
 
Migodi yote miwili North Mara na Bulyanhulu, uzalishaji wake umekuwa ukiongezeka, wakati North Mara ikifikia rekodi ya tani 505,000 za madini na udongo usiotakiwa zilizochimbwa kipindi cha robo mwaka kilichopita.Unaendelea kuboresha uchimbaji wa chini ya ardhi wakati mabadiliko ya mkakati wake wa uchimbaji yameongeza upanuzi wa migodi hii na kuanza uchimbaji katika mashimo ya wazi. Kwa upande wa Bulyanhulu, uendelezaji wa njia kuu za kufikia kina cha eneo la kuchimba madini ulianza kipindi cha robo mwaka kilichopita. Kuongezeka kwauzalishaji katika migodi yote miwili kumesaidiwa na uboreshaji wake.
 
“Tunaendelea kulenga ukuaji zaidi kupitia uchunguzi na kujumuisha leseni muhimu. Fursa za upanuzi zinatathminiwa katika maeneo ya Gokona na katika eneo zaidi la Bulyanhulu. Matokeo ya uchimbaji wa chini ya ardhi katika eneo la Gokona yanaonyesha matumaini ya kuongeza muda wa maisha ya Mgodi wa North Mara,” alisema Bristow.
 
“Kwa kuongezea uchunguzi wa maeneo yaliyoachwa uliobuniwa kudumisha mwelekeo chanya wa upanuzi wa rasilimali na kuzibadilisha katika migodi miwili, pia tunaangalia maeneo ya mbali zaidi. Uelewa mzuri zaidi wa usanifu wa kijiolojia tulio nao katika ukanda huo utaongeza uwezo wetu wa kugundua fursa mpya za maendeleo za daraja la kimataifa katika maeneo tuliyo na maslahi nayo.”
Kwa mujibu wa sera ya Barrick ya ajira za ndani, wazawa wa Tanzania, sasa wanafikia asilimia 96% ya wafanyakazi iliyowaajiri, huku asilimia 45% wakitokea katika jamii zinazozunguka migodi. Wazawa asilimia 58% wanashikilia nafasi za juu za uongozi. Katika robo ya mwaka iliyopita migodi ilitumia dola milioni $339 kwa kulipa wazabuni na watoa huduma wa Kitanzania. Tangu ilipotwaa migodi hiyo mwaka 2019, Barrick imechangia zaidi ya dola bilioni $2.1 katika uchumi wa Tanzania.
 
 
Akiongea kwa niaba ya Serikali katika mkutano huo,Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa aliipongeza kampuni ya Barrick kwa jitihada inazofanya kuhakikisha uwekezaji wake unachangia kukuza pato la Serikali sambamba na kuwezesha wananchi wanaoishi jirani na migodi yake kupitia miradi ya kijamii inayoitekeleza “Serikali tukiwa kama wabia wa Barrick kupitia kampuni ya Twiga tutahakikisha tunajenga mazingira mazuri zaidi ili raslimali ya madini iendelee kutoa mchango mkubwa zaidi katika kukuza uchumi wa Tanzania”.alisisitiza.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow akikabidhi mfano wa hundi ya dola 10,000 kwa Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Anger House Children’s Home, Holly Opondo (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika mkoani Mara . Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara,Bw.Yahya Nawanda
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, akikabidhi mfano wa hundi ya dola za 10,000 kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania Deaf Development Association, Kelvin Nyewa, wakati wa hafla iliyofanyika mkoani Mara . Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara,Bw.Yahya Nawanda (Kushoto)
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Corporation, Mark Bristow, akikabidhi mfano wa hundi ya dola za 10000 kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kahama Peace Orphanage Centre, Halima Hamza kwa ajili ya kusaidi kituo hicho wakati wa hafla iliyofanyika mkoani Mara . Wa pili ni Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, Bw.Yahya Nawanda (Kushoto)
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Bw. Mark Bristow, akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kuhusu mipango ya kampuni hiyo kupanua shughuli zake nchini uliofanyika North Mara mwishoni mwa wiki, Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, Yahya Nawanda (kushoto).
Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Mara wakimsikiliza Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (hayupo pichani), wakati akieleza mipango ya kampuni hiyo ya kuongeza uzalishaji wa dhahabu katika migodi ya Bulyanhulu na North Mara katika mkutano uliofanyika North Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, akiongozana na viongozi wa Mkoa wa Mara kutembelea mradi wa kilimo biashara wa vijana 100 uliowezeshwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara katika Kijiji cha Matongo mkoani wilayani Tarime.
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, akizungumza wakati wa mkutano
Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa akizungumza katika mkutano wa waandishi kuhusu mipango ya kampuni ya Barrick yenye ubia na Serikali kupitia Kampuni ya Twiga ya kuongeza uzalishaji wa dhahabu katika migodi ya North Mara na Bulyanhulu.

About the author

mzalendoeditor