Featured Kitaifa

TRA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA UTALII KATIKA ULIPAJI KODI.

Written by mzalendoeditor

Naibu kamishna wa idara ya kodi za ndani kutoka makao makuu Swalehe Byarugabe akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha katika kikao cha wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha.

…………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imekutana na wadau wa sekta ya utalii kwa lengo la kukaa pamoja na kuanzisha, kujadi na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabi katika suala zima la ulipaji kodi.
Akionhea na waandishi wa habari katika kikao cha wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha Naibu kamishna wa idara ya kodi za ndani kutoka makao makuu Swalehe Byarugabe alisema kuwa wapo katika mwendelezo wa kukutana na makundi ya walipa kodi lengo likiwa ni kusikiliza changamoto wanazokumbananazo zikiwemo za kibiashara pamoja na kikodi.
Alisema kuwa TRA imeendelea kuweka mikakati ulipaji kodi kwa wateja wake ili kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara wa Tanzania bara na visiwani wakiwemo wadau wa sekta hiyo ambao ni kundi muhimu la walipa kodi wakubwa na wa kati.
“Tumekuwa na taratibu za kusikiliza changamoto kwa makundi kwani kwa kufanya hivyo hali ya mapato nchini inazidi kuongezeka na hali hiyo ni matunda yatokanayo na ushirikiano baina ya TRA na wateja wake kutoka sekta mbalimbali,” Alisema Byarugabe.
Kwa upande wake Kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar Yusuph Mwenda alisema ushirikiano waliyonao ni moja ya kurahisisha ukusanyaji wa kodi kwa wateja wake ambapo sekta ya utalii kwa upande wa Zanzibar ndio unaoendesha uchumi kwa zaidi ya asilimia 40 hiyo mahusiano ya watalii wa bara huwa wanamalizia Tanzania Visiwani.
” Leo tumekutana jijini Arusha kuwasikiliza changamoto za wadau wa sekta ya utalii ambapo tutapata fursa ya kuwaeleza njia nzuri ya kurahisisha kufanya shughuli zao za utalii nchini kote bila usumbufu kwa pamoja na wageni wanaofika nchini,”alisema.
Hata hivyo baadhi ya wadau wa sekta ya utalii walisema mahali wanapoomba wafanyiwe marekebisho ni pamoja na mfumo wa ulipaji kodi pamoja na baadhi ya sera ambazo zimekuwa changamoto katika shughuli zao za utalii hiyo kupitia kikao hicho wataweza kuwaonyesha taswira kamili.
“Changamoto kubwa tuliyonayo kwa sasa ni changamoto ya kimfumu ambapo utaona VAT ya Tanzania bara ni asilimia 18 lakini ya Tanzania visiwani ni asilimia 15 ambapo pia hili tunataka tuliongelee ili tuweze kwenda sawa japo ni suala la kisera zaidi lakini tunaamini wataenda kuliwasilisha,” wakisema.
Naibu kamishna wa idara ya kodi za ndani kutoka makao makuu Swalehe Byarugabe akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha katika kikao cha wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha.
Kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar Yusuph Mwenda akiongea na waandishi wa habari katika kikao cha wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha.

About the author

mzalendoeditor