Burudani Featured

‘FANYENI OPERESHENI YA UHARAMIA’-WAZIRI MCHENGERWA

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa alitoa maelezo kwa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki na Kanuni kabla ya tarehe 01 Novemba, 2022 na kufanya operesheni ya uharamia, jana Oktoba 18, 2022 Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na DSTV na Azam Media.
……………………………..
Anitha Jonas – Ofisi ya Hakimiliki Tanzania
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki katika eneo la uharamia pamoja na Kanuni kabla ya tarehe 01/11/2022 na kufanya operesheni ya uharamia.
Mheshimiwa Mchengerwa ametoa agizo hilo jana Oktoba 18, 2022 Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na viongozi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania na Azam Media Ltd kufuatia malalamiko ya Kampuni hizo ya wizi wa maudhui.
“Suala la uharamia nafahamu kuwa limekithiri, Ofisi ya Hakimiliki toeni elimu kwa wadau na toeni matamko ya kukemea uharamia,”alisema Mhe.Mchengerwa.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho, Waziri huyo alisisitiza kuunda Kamati ya uharamia hivi karibuni ambayo itadhibiti uharamia.
Naye Muwakilishi wa Msimamizi wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania, Bw. Baraka Katemba alifafanua kuwa tayari Ofisi hiyo imeshandaa Kanuni hizo ambazo kama ilivyoelekezwa na Maboresho ya Sheria yanaendelea kufanyiwa kazi na ameahidi kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yatakamilika kwa wakati.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Multichoice Tanzania alieleza namna Kampuni hiyo inapata hasara kutokana na Uharamia wa maudhui wanayozalisha kutokana na baadhi ya wadau kurusha maudhui hayo bila kibali chao, pia alieleza namna Serikali inakosa mapato kutokana na baadhi ya wadau kutumia ving’amuzi ambavyo wanaviingiza kimagendo na kuvitumia kurusha matangazo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa alitoa maelezo kwa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki na Kanuni kabla ya tarehe 01 Novemba, 2022 na kufanya operesheni ya uharamia, jana Oktoba 18, 2022 Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na DSTV na Azam Media.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Multichoice Tanzania, Jackline Uisso (wanne kushoto)  pamoja Maafisa kutoka Azam Media mara baada ya kikao cha kujadili masuala ya uharamia kwa kazi za maudhui zinazozalishwa na vyombo hivyo jana Oktoba 18, 2022 Jijini Dar es Salaam.

About the author

mzalendoeditor