Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI DUGANGE AITAKA TSC KUENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (AFYA) Dkt. Festo Dugange,akizungumza wakati akifungua kikao cha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kilichofanyika leo  Oktoba 18, 2022 Jijini Dodoma.

………………………….

Na. Asila Twaha, OR – TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (AFYA) Dkt. Festo Dugange ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Tume hiyo.

Akifungua kikao cha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oktoba 18, 2022 Jijini Dodoma, Dkt. Dugange amewataka Watendaji wa Tume hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamamia utumishi wa walimu ambao ni zaidi ya asilimia 50 ya watumishi wa Umma nchini.

Dkt. Dugange Ameelezea na kutoa maelekezo kwa baadhi ya walimu kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa walimu kwa kufanya vitendo ambavyo havistahili katika utumishi ambapo jumla ya watumishi walimu 11,396 walichukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na walimu.

“ninaielekeza Tume kuendelea kuwachukulia hatua watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa walimu pale tu unapopatikana ushahidi usiotia shaka” amesisitiza Dkt. Dugange

Aidha, Dkt. Dugange ameitaka Tume hiyo kulifanyia kazi suala la utoro kwa walimu 7,579 kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu kwa sababu inaweza kusababisha walimu kutowajibika na kupelekea hasara kwa wananchi wanaohudumiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Bi. Paulina Mkwama ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuiamini Tume ya Utumishi wa Walimu pamoja na kushughulikia masuala ya kiutumishi wa walimu kwa kuajiri, kusajili walimu, kuwathibitisha kazini waliokidhi vigezo, kupandisha vyeo, kupandisha vyeo walimu waliojiendeleza, kushughulikia masuala ya kustaafu na kuelimisha walimu.

Aidha, ameiomba Serikali kuendelea kuangalia suala la Muundo wa Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kuwa muundo uliopo bado unaonyesha kuwa na uhitaji wa Makatibu Wasaidizi wa Wilaya ambao bado hawajateuliwa.

Bi. Mkwama pia amesema kuwa tayari mapendekezo ya mabadiliko ya muundo wa Maendeleo ya Utumishi na mshahara kwa watumishi wa Tume ulishawasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu ni kwa mujibu wa Kanuni ya 108 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 73 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2004.

Kikao hicho kina lengo la kuwaleta pamoja watumishi kwa kuwasilisha kero zao na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kujadili majukumu ya Tume ya Utumishi wa Walimu chenye kauli mbiu ya “Kazi Iendelee”

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (AFYA) Dkt. Festo Dugange,akizungumza wakati akifungua kikao cha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kilichofanyika leo  Oktoba 18, 2022 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Bi. Paulina Mkwama,akitoa taarifa ya kikao cha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kilichofanyika leo  Oktoba 18, 2022 Jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (AFYA) Dkt. Festo Dugange (hayupo pichani), wakati akifungua kikao cha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kilichofanyika leo  Oktoba 18, 2022 Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor