Yanga imeshindwa kuifuata Simba hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuchapwa bao 1_0 dhidi ya wenyeji Al Hilal mchezo uliopigwa uwanja wa Al Hilal nchini Sudan.
Al Hilal walipata bao dakika ya 3 likifungwa na Mohamed Abdelhaman baada ya makosa ya Bakar Mwamnyeto Yanga ametupwa nje kwa jumla ya mabao 2_1 mchezo wa awali timu zote zilitoka sare ya kufungana bao 1_1 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Sasa rasmi Yanga imeangukia Kombe la Shirikisho katika mtoani watacheza na timu zilizopo Kombe la Shirikisho.