Featured Michezo

VIPERS YATINGA MAKUNDI CAF,YAITOA TP MAZEMBE

Written by mzalendoeditor

TIMU ya TP Mazembe imeshindwa kutinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kutolewa kwa Mikwaju ya Penalti 4-2 na wageni Vipers kutoka nchini Uganda mchezo uliopigwa uwanja Stade TP Mazembe  uliopo Kamalondo Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 Mchezo wa kwanza nchini Uganda ulimalizika kwa sare ya bila kufungana hali kadhalika marudiano sare ya 0-0 hivyo kupelekea mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya Penalti.

Na Sasa TP Mazembe imeangukia Kwenye hatua ya Mtoani wa Kombe la Shirikisho barani Afrika

About the author

mzalendoeditor