Featured Kitaifa

MAJANGA YA MOTO NA DHARURA YAPATA MWAROBANI 

Written by mzalendoeditor

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi 

Ubalozi wa Uingereza na taasisi ya Mercy Coprps Pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam  kimetoa mafunzo ya namna gani ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii  na namna ya kuyakabilina na majanga hayo ikiwa ni Pamoja na mawasiliano Pale dharula inapotokea.

Akitoa maelezo Juu ya namna ya kukabiliana na Mjanga Mratibu wa shirika la Mercy Corps Nchini Bw. ANTHONY SAROTA amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa Jeshi la Polisi ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia hasa kwa upande wa mawasiliano Pale majanga yanapotokea.

kwa upande wake kamishna msaidizi wa Polisi ACP THABITHA MAKARANGA ambaye ni mratibu wa mafunzo hayo kwa upande wa Jeshi la Polisi, amesema Jeshi la Polisi linashukuru wawezeshaji wa mafunzo hayo na kusema kuwa mafunzo hayo yataleta tija na ufanisi kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na majanga ya dharura.

Akiongea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam kuanzia October 10 hadi 14  mwaka huu chini ya ufadhili wa ubalozi wa uingereza, taasisi ya mercy corps pamoja na wawezeshaji kutoka chuo kikuu dar es salaam, kamishna wa Polisi CP SHABANI HIKI amesema mafunzo hayo yatalisaidia kuwa jenga kiutendaji Aaskari wa  Jeshi la Polisi kwenye suala zima la kuboresha mawasiliano katika kukabiliana na Majanga na dharura

About the author

mzalendoeditor