Featured Kitaifa

KIGAHE ATETA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA INDORAMA COMMERCE DMCC YA INDIA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ikiwemo Aridhi, Amani na malighafi za kutosha hususani gesi asilia kwa viwanda vya ikkwemo utengenezaji wa mbolea.

Ameyasema hayo Oktoba 11, 2022 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Indorama Commerce DMCC ya India Bw. Venkatesh Gopalan na ujumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.

Wakijadikiana kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania Bw. Gopalan amesema Kampuni yake iko tayali kuja kiwekeza Tanzania hasa katika viwanda vya kutengeneza Mbolea kwa kutumia gesi asilia, sekta ya kilimo na madini.

Naye Naibu Waziri Kigahe aliwahahakikishia wawekezaji hao kuwa Serikali iko tayali kuwasaidia katika uwekezaji huo hususani viwanda vya mbolea kwa kutumia gesi asilia ili kuendeleza sekta ya kilimo inayoajiri Watanzania wengi na inayozalisha malighafi nyingi zinazojitajika viwandani kama vile pamba, katani, mbegu za mafuta ya kula na miwa inayotengeneza sukari.

About the author

mzalendoeditor