Na Odilo Bolgas MZALENDO BLOG
SIMBA ya Kimataifa Yaunguruma nchini Angola baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3_1 dhidi ya wenyeji Primiero de Agosto katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika .
Mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 8,beki Israel Mwenda dakika ya 63 na Moses Phiri dakika ya 76.
Wenyeji walipata bao la kufuatia machozi dakika ya 78 likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Dago.
Simba imejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya Makundi Mechi ya marudiano itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 16