TIMU ya Yanga imejiweka njia panda kutinga hatua ya makundi ya Michuano ya Klabu bingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wageni Al Hilal kutoka nchini Sudan mchezo uliomalizika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Yanga walipata bao kupitia Mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele dakika ya 50 huku n Al Hilal wakipata bao dakika ya 67 likifungwa na Mohamed Youseif aliyetokea benchi.
Kwa matokeo hayo Yanga wamejiweka katika nafasi finyu huku wakihitaji kwenda kushinda au kutoka sare ya kuanzia mabao 2 mchezo utakaopigwa mwishoni mwa wiki nchini Sudan.
Kama Yanga wataweza kutolewa wataangukia katika mtoani wa kombe la Shirikisho Afrika.