Featured Michezo

TAMISEMI YATAMBA KUFANYA VIZURI BAISKELI SHIMIWI

Written by mzalendoeditor

Na Asila Twaha, Tanga

TIMU ya Ofisi ya
Rais-TAMISEMI ya baiskeli kesho inaingia uwanjani katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) yanayoendelea jijini Tanga.

Timu ya TAMISEMI itawakilishwa na mchezaji wake mahiri, Joseph Masalu huku akiweka wazi mategemeo yake ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kilomita 50.

“ Nimejiandaa vizuri na matumini yangu makubwa kuwa nitafanya vizuri na kupeperusha vyema bendera ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.”

Katika mchezo wa leo, Oktoba 8, 2022 uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Ufundi (Tanga TECH), TAMISEMI Sports Club imeshiriki katika mchezo wa riadha kwa wanaume ambao ulishirikisha wanaridha mahiri Lukangaya Mazigo aliyekimbia mita 3000, Godfrey Duttu mita 800, Adolph Komba mita 100 na mita 200 na Elliot Nindi aliyekimbia mita 400.

Kwa upande wa mchezo wa kupokezana vijiti (Relay) mita 100 Joseph Masalu alishiriki kukimbia wakati katika mchezo wa kurusha tufe TAMISEMI iliwakilishwa na Jeremia Maswaga aliwakilisha vema kwa urushaji wa kiumahiri kwa mzunguko wa kwanza kupata mita 7.67 na kwa hatua ya pili mita 7.44.

About the author

mzalendoeditor