Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU AZINDUA MKAKATI WA NGOs JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa KITAIFA wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma.

 …………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini  kuendelea kutimiza wajibu kwa kuzingatia uzalendo ili kulinda maslahi ya Serikali kwa kuzingatia Sera,Sheria na Kanuni ili kukidhi malengo ya kuanzishwa kwa mashirika hayo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa KITAIFA wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS) ambapo amesema mashirika ni kiungo muhimu Katika kuleta tija kwa Jamii.

Waziri Mkuu amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatakiwa kuboresha Mawasiliano na Mamlaka za Serikali za Mitaa maeneo mlipo, kutoa taarifa sahihi ya shughuli wanazozifanya ili kuimarisha dhana ya uwazi na uwajibikaji na amezitaka Wizara, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa zihakikishe NGOs zinafanya kazi kulingana na usajili, malengo na vipaumbele vya Taifa

“NGOs zijielekeze kufanya kazi maeneo yenye uhitaji hususani vijijini badala ya kujitikita maeneo ya miji pekee na “NGOs ziendelee kubuni miradi endelevu ili ziweze kujiendesha na kupunguza na kuondoa kabisa utegemezi kwenye maeneo yanayotegemea fedha za nje” alisema Mhe. Majaliwa

“Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa zifutilie utekelezaji wa miradi na fedha zinazopatikana na kujiridhisha kwamba zinanufaisha wananchi na walengwa.” alisema Mhe. Majaliwa

Pia ameitaka Wizara kuanzisha Kitengo Maalum cha kufuatilia fedha za miradi zinazoletwa katika Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuweza kujua fedha hizo zinatekeleza vipi miradi hiyo kwa manufaa ya jamii ili hizio fedha zitumike kama zilivyokusudiwa kusiaida katika miradi mbalimbali nchini.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Mashirika hayo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii na ameyaomba Mashirika hayo kuanzisha Ofisi zao katika Makao Makuu ya Nchi Dodoma ili kurahisisha utendaji kazi katika ya Serikali na Mashirika hayo.

Amezitaka Wizara za Kisekta ambazo hazijaanzisha Madawati ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuyaanzisha ili yaweze kusaidia Uratibu wa NGOs zinazofanywa kazi katika Sekta mbalimbali nchini ili ziweke kutekeleza miradi na kutoa huduma kwa jamii.

Aidha ametoa rai kwa Wakurugenzi na wafanyakazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sera na Sheria zilizopo ili kuweza kufanikisha miradi.

Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hufanyika kila mwaka likikutanisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa lengo la kujadliana na kupeena mrejesho wa mafanikio ya Mwakla mzima ya Mashirika hayo na kujadili changamoto zilizopo katika Utekelezaji wa miradi mbalimbali na namna ya kuzitatua kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Waziri  wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amesema kuwa mkakati huo umeanza kufanyiwa kazi mwaka 2021 na sasa umekamilika na utakabidhiwa kwa wadau wote kwa utekelezaji.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mwantumu Mahiza, amezitaka asasi za kiraia nchini kufanya kazi kwa uzalendo na serikali itaendelea kuzifanyi kazi changamoto mbalimbali zinazo ikabili sekta hiyo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akikagua Banda la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati wa Kilele cha Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika Oktoba 04, 2022 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Msaada wa Kisheria (LSF) Lulu Ng’wanakilala kuhusu machapisho mbalimbali yanayotolewa na Asasi hiyo katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma , Oktoba 4, 2022. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mtoto mwenye ulemavu Chipowenga Zayeye, wa pili kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima na wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi, katika wa Maonesho ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, Oktoba 4, 2022 Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa KITAIFA wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akieleza lengo la Jukwaa la Mwaka la NGOs katika Kilele cha Jukwaa hilo kilichofanyika leo Oktoba 04, 2022 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa Kaitaifa wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akizindua Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na Madawati ya Uratibu wa NGOs katika Wizara za Kisekta wakati wa wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa Kaitaifa wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Doroth Gwajima Tuzo kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa Kitaifa  wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Mwantumu Mahiza  kulia ni Mwenyekiti wa NaCONGO, Dkt. Lilian Badi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akitoa cheti kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kilichoandaa Mkakati wa Taifa wa Uendeelvu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Nesia Mahenge wakati wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa Kitaifa   wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mara baada ya kumalizika kwa Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa Kitaifa   wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali (NSNS)uliofanyika leo Oktoba 4,2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor