Featured Kitaifa

WATU BINAFSI WATAKIWA KUANZISHA VITUO VYA KUWAHUDUMIA WAZEE

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na Wazee kwenye Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

……………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima,amesema kuwa ni wakati sasa kwa watu binafsi kuanzisha vituo vya kuwahudumia wazee kama ilivyo kwa maeneo mengine.

Waziri Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo leo Oktoba 02, 2022 wakati wa Kongamano la Wazee kuelekea Kilele cha Siku ya Wazee lililofanyika kwenye Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Dkt.Gwajima amesema kuwa kwa sasa wanasuka mpango wa huduma kwa wote ambao utakwenda kusaidia maboresho makubwa ya jinsi ya kuwahudumia watu.

”Kwa sasa  Sera ya wazee  inafanyiwa mapitio kwa ajili ya kuiboresha iweze kuendana na hali ya sasa huku wakiendelea kuusuka upya mpango wa huduma kwa wazee.”amesema Dk.Gwajima

Kuhusu makazi ya wazee amesema kuwa yanafanyia ukarabati mkubwa karibu nchi nzima ili yawe kwenye ubora unaotakiwa na kuepusha uvamizi kwa watu ambao wamekuwa kila wakati wakiyanyemelea.

Aidha amewaomba wazee kubadilisha hadithi za kale walizo wasimulia wajukuu zao kuhusiana na Imani za kishirikina na badala yake wakawahadithie hadithi zitakazowajenga na kuwa raia wema kwa taifa.

“Wazee wangu niwaombe sana, kama kuna baadhi yenu waliwahi kuwahadithia wajukuu juu ya Habari za kishirikina huko nyuma na kuchochea Vitendo vya Ukatili basi ni wakati wa kuwabadili Fikra kwa kuwapa hadithi zitakazo wafanya kuwa Raia wema kwa Taifa lao” amesema  Dkt. Gwajima

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bibi Amina Mfaki amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za Wazee ikiwepo kuwepo kwa madirisha ya Wazee kwenye maeneo ya kutolea huduma za Afya sambamba na upatikanaji wa Vitambulisho vya msamaha wa Matibabu kwa Wazee pamoja na wengine kukatiwa Bima ya Afya ya jamii.

“Zaidi ya Wazee Millioni 2.1 wametambuliwa na zaidi ya Wazee 500,000 wamepatiwa vitambulisho vya Bima ya Afya” amesema Bibi Amina.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Lameck Sengo ameiomba Serikali kuona suala la kuwashirikisha kwenye vyombo vya maamuzi linatekelezwa kwani kuwepo na uwakilishi katika vyombo hivyo husaidia wazee sauti yao kusikika.

“Katika Sensa ya 2012 sisi Wazee tulikuwa Milioni 2.5 na tunaimani kwenye Sensa ya Mwaka huu tutaongezeka zaidi kutokana na Serikali yetu kutuboreshea huduma zetu hivyo kama Baraza la Wazee limekamilika ni wakati muafaka sasa kupata uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.” amesema Mzee Lameck.

Makundi Maalum Dk. Doroth Gwajima, kuchukua hatua kufuatia baadhi ya watu kuvamiwa eneo la Makazi ya wazee Nunge Kigamboni mkoani Dar es Saalam na kujenda vibanda vya biashara na makazi.

Mwenyeketiki wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam Salum Abdallah Matimbwa,amemuomba Waziri Gwajima mara Sera ya wazee itakapo kamilika awasaidie kuwasimamia ili iwe sheria.

“Tunachoweza kuona umetusaidia ni kuisimamia Sera ya wazee ili izae sheria ambayo kwani kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu hata tunashindwa kusimamia kile tunachokitaka kwa muda mrefu” amesema Matimbwa.

Maazimisho ya siku ya wazee duniani nchini yatafikia kilele kesho ambapo Kitaifa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atazungumza na wazee jijini Dodoma

WAZIRI  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na Wazee kwenye Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima .akisisitiza jambo kwa na Wazee kwenye Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Amina Mfaki akitoa salam za Wizara hiyo wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la l Wazee Lameck Sendo akitoa salaam za Wazee wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Baadhi ya Wazee walishiriki kwenye Kongamano kueleke Siku ya Wazee wakiwa wanafuatilia mada mbalimbali wakati Kongamano lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Mwenyeketiki wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam Salum Abdallah Matimbwa,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wazee kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima (hayupo pichani) mara baada ya kuzngumza na Wazee kwenye Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima akikagua huduma za Afya zinazotolewa kwa Wazee wakati Kongamano lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Wazee wakati wa Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na Wazee mara baada ya kuzungumza kwenye Kongamano kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee lililofanyika leo Octoba 2,2022 kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor