Featured Kitaifa

DREAMS DEFENDER WAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi wetu,Ngorongoro, Arusha.

Taasisi ya Dreams Defender chini ya Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Leodger Leonard ( Kachebonaho) wameungana na wadau wa Utalii na mashirika mbalimbali kuadhimisha siku ya Utalii Duniani.

Taasisi hiyo katika kuadhimisha siku ya Utalii Duniani imefanikiwa kuandaa kongamano la vijana lilofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro Tourism Conference Centre Jikonii Arusha, Tanzania na kuweza kuhudhuriwa na vijana kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi kama Kazakhstan, Kenya, Uganda.

Kupitia Kongamano hilo vijana waliweza walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya kukuza na kuendelea sekta ya Utalii na namna ambavyo vijana wataendelea kunufaika na sekta hiyo kwa kupanua wigo wa fursa zaidi za ajira.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dreams Defender Ndgu Leodger Leonard ( Kachebonaho) amepongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo wameweza kuinua tena kwa kasi sekta ya Utalii toka janga la Uviko-19 kuisha ambapo kwa kupitia Filamu ya “Tanzania Royal Tour” imeweza kuhamasisha makundi mbalimbali ya watalii kutoka nchi tofauti kutembelea Tanzania na kuangalia vivutio vya kipekee vinavyopatikana nchini.

About the author

mzalendoeditor