Featured Kitaifa

WADAU WAJIFUNGIA DODOMA KUJADILI MASUALA YA DIASPORA NA USHIRIKIANO WAO KATIKA MAENDEKEO YA TAIFA

Written by mzalendoeditor

KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

WIZARA ya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mapendekezo kwa Serikali kuhusu hadhi maalum ambayo  itaongeza ushiriki zaidi kwa Diaspora katika shughuli za maendeleo.

Pia imesema imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kutengeneza mazingira wezeshi  ya kuvutia na kuongeza shauku ya Diaspora wa Tanzania kushirikiana na kukuza uchumi wa Nchi.

Hayo yameelezwa  leo Septemba 29 Jijini,2022 na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola,wakati akifungua Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

Balozi Kayola,amesema  kupitia mikutano ya wadau kama makongamano ya Diaspora na mikutano mingine uratibu wa Diaspora umeendelea kufanyika ili kupokea changamoto na kuzitafutia masuluhisho haraka.

“Kupitia dhamira hiyo Wizara yetu ipo katika hatua za mwisho kukamilisha mapendekezo kwa Serikali kuhusu hadhi maalum ambayo tunaamini itaongeza ushiriki zaidi kwa Diaspora katika shughuli za maendeleo,”amesema Balozi Kayola

Balozi Kayola, amesema  Septemba 22 mwaka huu Wizara ilisaini hati ya makubaliano na mkandarasi kwa ajili ya kuanza matengenezo ya mfumo wa kidigital wa kuhifadhi taarifa  zote muhimu wa watanzania wanaoishi  na kufanya kazi nje ya Nchi ujulikanao kama Diaspora Digital Hub.

“Mfumo huu pamoja na mambo mengine utasaidia katika kuunganisha kushirikisha na kuhamasisha watanzania wote wanaoishi  na kufanya kazi nje ya nchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa letu,”amesema Balozi Kayola.

Vilevile,utatumiwa na wadau wanaohusika na masuala ya Diaspora hapa nchini kama dirisha maalum la kutambua na kusajili na kutoa huduma zao kwa Diaspora Kidigital.

Pia, amesema Serikali  imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kutengeneza mazingira wezeshi  ya kuvutia na kuongeza shauku ya Diaspora wa Tanzania kushirikiana na kukuza uchumi wa nchi.

Jitihada hizo ni pamoja na mwaka 2010 kuanzishwa kwa kitengo cha Diaspora chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kwa  Zanzibar ilianzishwa Idara ya ushirikiano wa Kimataifa  na uratibu wa masuala ya Diaspora.

Amesema jukumu kubwa la ofisi hizo ni kusimamia uratibu na kushughulikia masuala yote ya yanayohusu ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo ya Tanzania.

Hata hivyo Serikali imewashauri wadau  kwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita kutekeleza kwa pamoja dhamira ya uendelezaji  wa miradi ya ujenzi  wa majengo ya vitega uchumi kupitia miradi yenye ubia wenye faida katika viwanja wa Balozi nje ya Nchi.

“Karibuni Wizarani tuzungumze namna namna ya ushirikiano wa ubia katika kufanikisha miradi hii muhimu ya kimkakati,”amesema

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi,Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora,Ofisi ya Rais -Ikulu Zanzibar Bi.Maryam Ramadhan Hamoud,amesema kuwa wadau watazungumzia mchango wa Diaspotra katika sekta za Afya,Elimu,Uwekezaji na umuhimu wa Diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fedha wanazotuma nyumbani.

”Wadau watapata fursa ya kutambua huduma mbalimbali za misaada ya kijamii,Sayansi na Ubunifu,ambayo huletwa nchini na wafadhili kupitia uratibu wa Diaspora”amesema Bi.Hamoud,

Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi James Bwana,amesema kupitia mkutano huo Serikali pamoja na wadau wa Sekta binafsi wataweza kujadili namna mataifa mengine duniani yalinyofanikiwa katika eneo la ushirikishwaji wa diaspora.

”Mkutano huo umezikutanisha taasisi za fedha,kampuni za simu za mikononi,taasisi za umma na binafsi za ujenzi wa nyumba na makazi,Shirika la nyumba la Taifa (NHC),Hamidu City Park,KC Land”amesema

KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi James Bwana,akitoa mada wakati wa Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Kaimu  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola (hayupo pichani)  wakati akifungua Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

Naibu Mkurugenzi,Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora,Ofisi ya Rais -Ikulu Zanzibar Bi.Maryam Ramadhan Hamoud,akizungumza wakati  wa Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

 

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni ya KC Land Development Plan Khalid Chanzi ,akizungumza wakati  wa Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya Diaspora na ushirikishwaji wao katika maendeleo ya Taifa ulioanza leo tarehe 26 hadi 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor