Featured Kitaifa

WATUHUMIWA 15 MBARONI KWA MAUAJI TUNDURU MKOANI RUVUMA

Written by mzalendoeditor

Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi, Tunduru -Ruvuma

Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo Nchini limesema linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Hayo ya mesemwa leo September 24 2022 na kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA alipofika Kijiji cha mbatamila wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa kumi na tano (15) kwa kosa la mauaji ya vijana wanne wa familia moja katika Kijiji cha mbatamila nakusema kuwa wale wote waliofanya mauaji hayo hawako salama nakuwataka wajisalimishe Jeshi la Polisi.

Aidha amewataka wakulima na wafugaji kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate misingi ya sheria na taratibu katika kutatua Changamoto zilizopo.

Sambamba na hilo amewapa Pole wananchi waliopoteza ndugu zao ambapo kamanda Pasua amesema Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote walio baki ili wafikiahwe katika vyombo sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

KUKAMATWA KWA MIFUGO 159 ILIYOIBIWA MBATAMILA WILAYA TUNDURU MKOA WA RUVUMA

Pia kamanda Pasua amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mifugo 159 iliyokuwa imeibiwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea kushrikiana na wafugaji na wakulima katika kupambana nauhalifu wowote ule.

Kwa upande wake katibu wa chama cha wafugaji Nchini Bi. Prisca Kaponda amesema wao kama chama cha wafugaji kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakuliama nawafugaji hapa nchini.

Nao baadhi ya wahanga wa tukio hilo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa jitihada walizo chukua za kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya mauaji na kukamata mifugo ilikuwa imeibiwa katika Kijiji cha mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma na kuliomba Jeshi hilo kuweka nguvu kubwa ili kupata mifugo ambayo haijapatikana.

About the author

mzalendoeditor