Featured Kitaifa

TBS YAWAPA NENO WAKANDARASI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Afisa Viwango kutoka Shirika Viwango Tanzania (TBS) Innocent Johnbosco  akizungumza na Waandishi wa Habari katika banda la Shirika hilo  wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya Wahandisi yanayofanyika jijini Dodoma.

…………………………….

Na Alex Sonna _DODOMA

WAKANDARASI wameshauriwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kulinda ubora wa kile wanachotengeneza.

Ushauri huo umetolewa leo Septemba 23,2022 na  Afisa Viwango kutoka Shirika Viwango Tanzania (TBS)Innocent Johnbosco  akizungumza na Waandishi wa Habari katika banda la Shirika hilo  wakati wa maadhimisho ya 19 ya siku ya Wahandisi inayofanyika jijini Dodoma.

Johnbosco amesema katika siku ya Wahandisi Tanzania TBS wameshiriki kuendelea kuwahamasisha Wahandisi katika kutoa elimu juu ya viwango vinavyohusiana na project mbalimbali.

“Pia tunaendelea kuhamasisha Wakandarasi kuzalisha na kutumia bidhaa zilizothibitishwa na TBS,”amesema Johnbosco.

Amesema wanaendelea kuwahamasisha wajasiriamali wadogo wadogo waweze kupata nembo za ubora na zinazokidhi viwango ili kumlinda mlaji na kuimarisha uchumi wa Nchi.

About the author

mzalendoeditor