Featured Kitaifa

MAJALIWA AZINDUA MWONGOZO WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA USTAWI WA JAMII

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Kaptain Mstaafu George Mkuchika,akizindua Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa uliofanyika leo Septemba 23,2022 jijini Dodoma.

……………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imezitaka Wizara zinazohusika na utekelezaji wa Mwongozo wa Mpango Kabambe wa Afua za Ustawi wa Jamii kuhakikisha zinasimamia urasimishwaji na utekelezaji wa mwongozo huo katika jamii.

Agizo hilo limetolewa leo Septemba 23,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Kaptain Mstaafu George Mkuchika wakati akizindua Mwongozo huo niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Mhe.Mkuchika amesema utekelezaji wa Afua za Ustawi wa Jamii ni suala mtambuka linalotekelezwa na Wadau tofauti hivyo mwongozo huo utatumiwa na Wadau wa kisekta wanaotoa Huduma za Ustawi katika kuhakikisha Mipango na bajeti zao zinaakisi Mipango na vipaumbele vya Serikali.

“Mwongozo huu pia utasaidia katika upangaji wa Mipango, bajeti pamoja na upatikanaji wa taarifa mbalimbali zinazowahusu watoto, watu wenye ulemavu, Wazee na Makundi Maalum” amesema Mhe. Mkuchika.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mwongozo huu utachochea kwa kiasi kikubwa kasi ya utoaji na upatikanaji wa Huduma Bora za Ustawi wa Jamii kwa Makundi Maalum na hivyo kujenga mustakabali imara wa Jamii ya kitanzania katika kufikia matarajio yao

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema mwongozo huo utaimarisha mfumo wa ukusanyaji wa takwimu za Huduma za Ustawi wa Jamii na kujumuishwa katika mfumo wa kidijitali wa Mipango na Taarifa.

Ameziagiza pia Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kukusanya takwimu na kuandaa mipango na bajeti za Ustawi wa Jamii kwa mujibu wa mwongozo huo.

“Mwongozo usimamiwe kikamilifu ili kuwezesha utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba Jamii ikiwemo ukatili wa kijinsia hasa Wanawake na watoto, mauaji na matukio ya kujiua katika Jamii na ongezeko la watoto wa mitaani” Mhe. Mkuchika

Kwa upande wake  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema lengo la kuzindua mwongozo huo ni kuimarisha utoaji wa huduma kwa Makundi Maalum ikiwemo Wazee, Walemavu, Watu wenye magonjwa sugu, Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na makundi mengine yenye mahitaji maalum.

“Kumekuwa na ukatili mwingi unaoendelea kwenye jamii na kazi kubwa inafanywa kuhakikisha wananchi wanaelewa haki zao tofauti na mwanzo, tmeenda mbele zaidi tuna jeshi la jamii linayojulikana kama SMAUJATA nitoe wito kwa wananchi kujiunga na niwapongeze Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kwa kazi kubwa” amesema Mhe. Dkt. Gwajima.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Sinyamule ameshukuru kwa niaba ya watekelezaji wa mwongozo huu na kusema kwamba utakuwa kitendea kazi muhimu kwa wao kufanyia kazi ili kuhakikisha Makundi Maalum yanapata Huduma zinazostahili.

“Nazipongeza Wizara kwa kuanzisha mwongozo huu ambao utaunganiza sekta mbalimba katika kutatua changamoto za Makundi haya” amesema Mhe. Sinyamule.

Mwongozo huu unatekelezwa na Wizara Taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Fedha na Mipango, Mambo ya Ndani, Katiba na Sheria, Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Afya.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Kazi Maalum ,Mhe Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii uliofanyika leo Septemba 23,2o22 jijini  Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa  uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua za Ustawi wa Jamii uliofanyika leo Septemba 23,2022 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa USAID ,Kate Somvongsiri akizungumza kwenye Hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii uliofanyika  leo Septemba 23,2022 jijini  Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akizungumza kwenye Hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii uliofanyika  leo Septemba 23,2022 jijini  Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii uliofanyika  leo Septemba 23,2022 jijini  Dodoma.

Sehemu ya washiriki Mbalimbali wakifatilia hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii uliofanyika  leo Septemba 23,2022 jijini  Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Kaptain Mstaafu George Mkuchika,akizindua Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa uliofanyika leo Septemba 23,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Kaptain Mstaafu George Mkuchika,akimkabidhi nakala ya Mwongozo Katika hafla ya Uzinduzi wa Mwongozo wa Mpango Kabambe wa Afua za Ustawi Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima mara baada ya kuuzindua  kwa inaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa uliofanyika leo Septemba 23,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe. Kaptain Mstaafu George Mkuchika,akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua Mwongozo wa Mpango Kabambe Wa Afua Za Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa uliofanyika leo Septemba 23,2022 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor