Featured Kitaifa

WAJASIRIAMALI 25O KUSHIRIKI MAONYESHO YA 22 YA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NCHINI UGANDA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu wajasiriamali watakaoshiriki Maonesho ya 22 ya wajasiriamali wadogo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 8-18 ,mwaka huo.

………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAJASILIAMALI Wadogo na wa Kati 250 wanatarajia kushiriki Maonesho ya 22 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali yatakayofanyika Jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 8 hadi 18 mwezi Desemba 2022. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako,amesema kuwa Wajasiriamali watakaoshiriki wanatakiwa kupeleka bidhaa za asili za Mikoa au Wilaya wanazotoka.

Prof.Ndalichako amesema kuwa serikali imejipanga kuwawezesha vijana wajasirimali wa Tanzania kushiriki na itatoa kipaumbele kwa watakaozalisha bidhaa za Tanzania zenye ubora unaokishi soko la Jumuiya hiyo.

” Ninapenda kusisitiza kwa wahusika wote kuhakikisha wanawaibua na kuwateua vijana wajasiriamali kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.Maonesho haya hufanyika sambamba na mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali kuhusu masoko; Ubora wa bidhaa; Urasimishaji biashara; na Kuongeza  thamani ya bidhaa”amesema Prof.Ndalichako

Waziri Ndalichako amesema kuwa katika kipindi cha miaka mingi, pamoja na mambo mengine, serikali imekua ikichangia usafiri wa mizigo ya Wajasiriamali kwenda kwenye maonesho hayo.

”Kwa mwaka huu, Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Rais Samia imepanga kuongeza mchango wake kwa kuwezesha usafiri wa basi la wajasiriamali kwenda na kurudi Uganda“ameeleza

Hata hivyo  Prof.Ndalichako amesema kuwa Wizara yake itafungua dirisha la maombi ya vijana wajasirimali wanaotaka kushiriki maonesho hayo kuanzia Septemba 26 hadi Oktoba 17 mwaka huu.

”Wanaokusudia kushiriki watachukua fomu katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kote nchini, kupitia tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu: www.kazi.go.tz na Ofisi za Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo (CISO (T).”amesema Prof.Ndalichako

Aidha,amesema kuwa fomu hizo pia zitapatikana kupitia Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo ila zote zitapaswa kurudishwa kupitia Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa. 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Wajasiriamali Wadogo Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Joseph Rweyemamu, amesema kuwa wajasiriamali wapatao 1,000 kutoka Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Tanzania  watashiriki maonesho hayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu wajasiriamali watakaoshiriki Maonesho ya 22 ya wajasiriamali wadogo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 8-18 ,mwaka huo.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa   na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu wajasiriamali watakaoshiriki Maonesho ya 22 ya wajasiriamali wadogo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 8-18 ,mwaka huo.

Mwenyekiti wa shirikisho la Vyama Vya Wajasiriamali Wadogo Tanzania Bw. Josephat Rweyemamu ,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wajasiriamali watakaoshiriki Maonesho ya 22 ya wajasiriamali wadogo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Kampala nchini Uganda kuanzia Desemba 8-18 ,mwaka huo.

About the author

mzalendoeditor