Featured Kitaifa

SERIKALI YATENGA SH.BILIONI 100 UJENZI WA VETA NCHINI-WAZIRI MKENDA

Written by mzalendoeditor

Na
Mathias Canal, WEST-Dodoma

Serikali inayo azma ya kujenga
Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka huu wa fedha
2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni Mia moja (100 Bil).

Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili
ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo
zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi. Aidha, Wilaya ya Manyoni ni
miongoni mwa Wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya
Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema hayo leo tarehe 21 Septemba 2022 Bungeni
Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa
Jimbo Manyoni Mashariki
aliyetaka
kufahamu serikali ina Mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Wilayani Manyoni

Waziri Mkenda amesema kuwa katika
mwaka huu wa fedha 2022/23, Serikali imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili
ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo
zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi.

Aidha, Prof Mkenda amesema kuwa Wilaya
ya Manyoni ni miongoni mwa Wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa
kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.

Waziri Mkenda amewashauri wananchi
wa wilaya ya Manyoni wakiwemo wa Jimbo la Manyoni Mashariki waendelee kutumia  Chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa Singida, na
Chuo cha Wilaya ya Ikungi, Pamoja na Vyuo vya Singida na Msingi FDC  na Vyuo vingine vya ufundi stadi vilivyopo
nchini.


About the author

mzalendoeditor