Featured Kitaifa

“OPERESHENI YA KUKABILIANA NA PANYA ROAD IMEKUWA NA MANUFAA MAKUBWA”__RC MAkalla

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa Wa Dar es salaam Amosi Makalla amesema kwa Siku nne tangu kuanza kwa Operesheni ya kukabiliana na Panya Road Mkoa upo salama baada ya kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 135 na vifaa mbalimbali vulivyoibiwa.

Ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha Kamati ya ulinzi na usalama kilichoketi kufanya tathmini ya hali ya usalama Mkoa Wa Dar es Salaam pamoja na kupokea taarifa ya mwenendo wa uparesheni ya kukamata wahalifu leo 19 Septemba, 2022

Rc Makalla amesema mipango ya kudhibiti uhalifu ikiwemo vituo vyote vya polisi kufanya kazi kwa saa 24, ongezeko la doria kila kata na kila Mtaa kufanya Mkutano maalumu kujadili ajenda ya ulinzi na usalama kila wiki ya kwanza ya mwezi.

“Wafanya biashara wanaouza na kununua vifaa vya wizi, kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi, ufuatiliaji wa mienendo wafungwa waliomaliza kutumikia vifungo na msako kwenye vijiwe, majumba mabovu yasiyokamilika ( mapagala) na vibanda umiza ambavyo vimekuwa sehemu ya kukutana na kuweka mipango”. Amesema Makalla.

Pamoja na hayo Makalla ametoa wito kwa Wazazi kuhakikisha wanazingatia suala la malezi kwa kufuatilia mienendo ya Watoto wao.

“Wazazi tuwe kipaumbele kwa kufuatilia mienendo ya Watoto wetu maana kama hufuatilii hata Mtoto akiharibika huwezi kujua, akifanya mambo ya ajabu huwezi kujua pia naomba tufuatilie watoto wetu kwa kila hatua”.Amesema Makalla

Ameongezea kwa kusema Operesheni ya kukamata Panya Road ilizinduliwa Septemba 15 na ndani ya siku nne imekuwa na mafanikio makubwa yaliyopelekea kukamatwa kwa Watuhumiwa 135, Wanunuzi 5 wa vifaa vya wizi na kupatikana kwa mali zilizoibiwa ikiwemo Yv, Radio, Simu za Mkononi na Vitu vingine.

About the author

mzalendoeditor