Featured Michezo

SIMBA YAFUZU RAUNDI YA KWANZA CAF,PHIRI AZIDI KUWASHA MOTO

Written by mzalendoeditor

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imefanikiwa imetinga raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets   na kufikia jumla ya mabao 4-0 baada ya mechii ya kwanza Simba Sc akiwa ugenini  kupata mabao 2-0.

Simba Sc imepata mabao kupitia kwa Moses Phiri ambaye amepachika mabao yote mawili na  kuiwezesha timu yake kutinga hatua inayofuata Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba Sc inatinga hatua inafuata na kuungana na wenzake Yanga Sc ambao nao jana walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwachapa Zalan Fc kwa jumla ya mabao 9-0.

About the author

mzalendoeditor