Featured Kitaifa

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA TISHA NA TEMBOCARD KANDA YA MAGHARIBI MJINI KAHAMA

Written by mzalendoeditor
 
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi 

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa (aliyevaa miwani kushoto) akifurahia wakati akizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi Mjini Kahama. Kulia ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’ yenye lengo la kuwahamasisha wateja na Watanzania kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya manunuzi na malipo ya huduma huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo kushuhudia kombe la Dunia Qatar.
 
Uzinduzi wa Kampeni ya Tisha na Tembocard Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Tabora, Shinyanga, Kigoma, Geita na wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza umefanyika leo Jumamosi Septemba 17,2022 katika Benki ya CRDB tawi la Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkusa ameipongeza Benki ya CRDB kwa Kampeni hiyo huku akiishukuru kuichagua Manispaa ya Kahama kuwa sehemu ya kuzindulia kampeni ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’ katika mikoa ya Kanda ya Magharibi.
 
“Tunawashukuru Benki ya CRDB kwa kutupa heshima hii hapa Manispaa ya Kahama na hii inatokana pia na kwamba Kahama ni kitovu cha biashara. Tunaamini kati ya washindi wataokwenda Qatar watatoka Kahama.
 
Kahama inaunganisha nchi mbalimbali, wafanyabiashara wengi wanapita hapa, wanalala hapa hivyo kutokana na huduma hii pesa zao zitakuwa salama. Tunawapongeza sana Benki ya CRDB kwa kuendelea kukimbia Kidijitali”, amesema Mkusa.
 
Ameipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu wa kuwarahisishia wateja wake kupata huduma mbalimbali huku akiwashauri wananchi kutumia huduma hiyo badala ya kutembea na pesa taslimu hali ambayo ni inahatarisha usalama wa fedha zao.
 
Kwa upande Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana amesema Tisha na Tembocard inawarahisishia wananchi kupata huduma bila kutembea na fedha taslimu huku wakijishindia zawadi.
 
Amezitaja zawadi hizo kuwa ni fedha taslimu kila mwezi kwa wateja watatu ambapo watajishindia Sh. Milioni moja kwa mshindi wa kwanza, wengine washindi wawili watapata Sh.500,000 .
 
“Na kubwa zaidi ni safari ya kwenda nchini Qatar kuhushuhudia Kombe la Dunia iliyolipiwa kila kitu kwa wateja wanne wa TemboCard, washindi ni wale tu watakaokuwa na miamala mingi kupitia kadi zao za TemboCard”, amesema.
 
Amesema Tisha na Tembocard ni mkakati wa benki ya CRDB kujenga jamii yenye matumizi machache ya pesa taslimu ‘Cashless society’.
 
“Hakuna tena haja ya kutembea na maburungutu ya fedha na hakuna makato. Nchi za wenzetu hawatembei na fedha taslimu. Wajanja hawabebi Cash!. Kupitia Tisha na TemboCard mteja atakuwa akihitaji huduma au bidhaa anatumia kadi yake kuchanja tu na kulipia badala ya kutoa burungutu la fedha”,ameongeza Wagana.
 
“Tisha na Tembocard itakuwezesha kulipia manunuzi na huduma katika maduka, supermarkets, migahawa, hoteli na vituo vya mafuta kupitia vifaa vya manunuzi (POS), pamoja na malipo ya mitandaoni ikiwamo kulipia tiketi za ndege au malipo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi”,ameeleza Wagana.
 
Wagana amewashauri wateja wote wenye kadi za TemboCard kufurahia urahisi wa kufanya malipo popote pale walipo huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi na wateja ambao hawana akaunti katika Benki ya CRDB huu ndiyo wakati wa kufungua akaunti na kuanza kuweka fedha ili kurahisisha kufanya miamala kupitia TemboCard zao ambazo watapewa baada ya kufungua akaunti.
 
Naye Balozi wa Benki ya CRDB nchini Tanzania,Isabella Mwampamba amesema Benki ya CRDB ni Benki pendwa ya Kizalendo hivyo kuwaomba wananchi kuchangamkia huduma hiyo akisema ‘Tisha na Tembocard ndiyo habari ya mjini!’.
 
Nao baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo Mwakilishi wa The Planet Hotel, Eveline Yohana na Meneja wa Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, Esther John wameishukuru benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya Tisha na Tembocard ambayo ni rahisi, salama na kupunguza muda wa kubeba fedha nyingi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa akizungumza wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  Mjini Kahama leo Jumamosi Septemba 17,2022 katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama.  Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa akizungumza wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  Mjini Kahama leo Jumamosi Septemba 17,2022 katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama. 
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’ Kanda ya Magharibi Mjini Kahama leo Jumamosi Septemba 17,2022 katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama. 

Balozi wa Benki ya CRDB nchini Tanzania,Isabella Mwampamba akizungumza wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  Mjini Kahama. 
Balozi wa Benki ya CRDB nchini Tanzania,Isabella Mwampamba akizungumza wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  Mjini Kahama.
Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kahama, Dorcas Ngowi akizungumza wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  Mjini Kahama.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa (kushoto) akizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi Mjini Kahama. Kulia ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa (aliyevaa miwani kushoto) akizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi Mjini Kahama. Kulia ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa (kushoto) akifurahia wakati akizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi Mjini Kahama. Kulia ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa (aliyevaa miwani kushoto) akifurahia wakati akizindua Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi Mjini Kahama. Kulia ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa akipiga picha ya pamoja na sehemu ya wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi 
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi 
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Clemence Mkusa akipiga picha ya pamoja na wateja na wafanyakazi wa benki ya CRDB wakati wa uzinduzi Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’  CRDB Kanda ya Magharibi 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kahama Social, Bahini Martine Mitundwa akizungumza baada ya uzinduzi wa Kampeni Maalum ya Matumizi ya Kadi maarufu ‘Tisha na TemboCard’ 
Mwakilishi wa The Planet Hotel  akiishukuru benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya Tisha na Tembocard
Meneja wa Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, Esther John akiishukuru benki ya CRDB kwa kuanzisha huduma ya Tisha na Tembocard
 
Meneja wa Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, Esther John  akimhudumia kupitia Tembocard Balozi wa Benki ya CRDB nchini Tanzania,Isabella Mwampamba aliyefika katika kituo hicho cha mafuta kupata huduma ya kujaziwa mafuta kwenye gari lake.

Mfanyakazi wa Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, Josephina Boniphace akimhudumia Balozi wa Benki ya CRDB nchini Tanzania,Isabella Mwampamba
Mfanyakazi wa Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, Josephina Boniphace akimhudumia Balozi wa Benki ya CRDB nchini Tanzania,Isabella Mwampamba
Meneja wa Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akiwa kwenye kituo cha Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, na kujionea jinsi wanavyotoa huduma kupitia CRDB Tembocard
Meneja wa Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akiwa kwenye kituo cha Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama, na kujionea jinsi wanavyotoa huduma kupitia CRDB Tembocard
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wadau wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kituo cha Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wadau wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kituo cha Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wadau wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kituo cha Kampuni ya mafuta ya Sasagi Oil Mjini Kahama.
 
Picha zote na Kadama Malunde  – Malunde 1 blog
 
About the author

mzalendoeditor