Featured Kitaifa

RAIS DK.DK.MWINYI AHUDHURIA MAZIKO YA ASKOFU MSTAFU WA KANISA LA ANGLIKANA MKUNAZINI ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar kuhudhuria maziko ya Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la  Anglikana  Zanzibar John Ramadhan, yaliyofanyika leo 17-9-2022, katika viwanja vya kanisa hilo Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihudhuria maziko ya Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar John Ramadhan, yaliofanyika katika Kanisa la Mkunazini leo 17-9-2022 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu Mhe. Georg Mkuchika na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Shaban.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar leo 17-9-2022. Maziko yaliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Anglikana Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Askofu Mstafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar John Ramadhan, maziko hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar l

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Viongozi wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa maziko ya Askofu Mstafu Marehemu John Ramadhan yaliofanyika leo 17-9- 2022 katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor