Featured Kitaifa

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA MABALOZI WATEULE WA FINLAND, CANADA NA HISPANIA

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amepokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wateule wa nchi za Finland, Hispania na Canada katika hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.
Mabalozi wateule waliowasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Mhe. Waziri Mulamula leo ni Balozi wa Canada Nchini, Mhe. Kyle Nunas, Balozi wa Finland Nchini, Mhe. Zitting Maria Theresa na Balozi wa Hispania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez.
 
Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti Mhe. Waziri amewaahidi kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu hapa nchini na kuwasihi kuendeleza kile ambacho mabalozi waliowatangulia wamekifanya katika nyanja mbalimbali za ushirikiano baina ya nchi zao na Tanzania.
 
Akizungumza baada ya kuwasilisha nakala ya hati zake kwa Mhe. Waziri, Balozi mteule wa Finland Mhe. Zitting Maria Theresa aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Finland na kuongeza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, masuala ya jinsia na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake.
 
Naye Balozi Mteule wa Canada Mhe. Kyle Nunas amesema Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuibua maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo biashara na uwekezaji, sekta ya madini,elimu , maji na ulinzi na usalama.
 
Naye Balozi Mteule wa Hispani Nchini, Mhe. Jorge Moragas Sanches amemuahidi Mhe. Waziri kuwa Hispania itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo, afya, michezo, maji, elimu na umeme vijijini ili kuleta tija nchini.
 
Katika hatua nyingine Balozi Mulamula amekutana na kuzungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende Malepe. Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamejadili jinsi ya kuendelea kushirikiana kwa kuzingatia makubaliano ambayo nchi hizi mbili ziliingia kwa lengo la kufungua maeneo zaidi ya ushirikiano kupitia fursa za kujengeana uwezo kati ya wananchi wa Tanzania na Afrika Kusini.
Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez.
Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe aliyekuja ofisini kwake kufanya mazungumzo kuhusu ushiikiano wa mataifa yao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe .

About the author

mzalendoeditor