Featured Michezo

UJENZI WA VIWANJA VYA MICHEZO NI JUKUMU LA SERIKALI NA WADAU

Written by mzalendoeditor

Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amesema ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi , Mashirika ya Umma na Wadau wa michezo.

Amesema hayo leo Septemba 16, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali wa Mhe. Shaban Omari Shekilindi (Lushoto) aliyeuliza Je ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo katika Mji wa Lushoto.

Napenda kutumia nafasi hii, kuzikumbusha Halmashauri nchini ikiwemo Halmashauri ya Lushoto, kuzingatia matakwa ya Sera ya Michezo kwa kutenga fedha  kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kukarabati na kujenga miundombinu ya michezo” amesema Mhe.Gekul.

Mhe.Gekul ameeleza kuwa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Mwaka 1995 ibara 7 inaeleza  jukumu la ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya michezo ni jukumu la watu wote na mazingira ya kuwekeza yameainishwa kwa uwazi.

About the author

mzalendoeditor