NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imefanikiwa kuichapa Tanzania Prison kwa bao la dakika za lala salama kupitia kwa kiungo wake Jonas Mkude akipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Kibu Denis dakika ya 86 ya mchezo.
Mchezo huo ambao ulichezawa katika dimba la Sokoine Mbeya, Tanzania Prison walikuwa wenyeji waliweza kuwazuia Simba kutopata bao kwa dakika zote kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili licha ya jitihada za kuzuia waliweza kufungwa bao moja.
Simba Sc imejikusanyia pointi 10 sawa na Yanga ambao hapo jana waliweza kushinda mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Yanga wanaongoza Msimamamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na Simba wanashika nafasi ya pili huku Azam FC wakishika nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 8.