Featured Kitaifa

JESHI LA POLISI NCHINI LATOA UFAFANUZI KUHUSU VIDEO INAYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Written by mzalendoeditor

 

Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa Katika mitandao ya kijamii imeonekana video fupi (clip) ikisambaa ambapo imekimwonyesha askari Polisi akichukua fedha kwa raia wa kigeni baada ya mazungumzo ambayo yalionyesha ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Jeshi la Polisi.

Akitoa ufafanuzi huo leo September 14 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME amesema kuwa Inawezekana wanao isambaza video hiyo hawakupata mrejesho wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya askari huyo aliyeendekeza tamaa zake binafsi na kufikia hatua hiyo ambayo ililifedhehesha Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla.

SACP Misime amebainisha kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea huko katika Mkoa wa Kaskazini Unguja miaka mitano iliyopita ambapo askari huyo alishtakiwa na ndani ya siku tatu alipatikana na hatia na alifukuzwa kazi kwa fedheha ili iwe fundisho kwa askari wengine wenye tabia kama hiyo.

Sambamba na hilo Misime amewaambia waandishi wa Habari kuwa Jeshi la Polisi linawahakikishia watanzania kuwa litaendelea kuwachukulia hatua kali askari yeyote yule wa Polisi ambaye hataki kubadilika na kuendekeza tamaa binafsi ambazo ni kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi Tanzania.

About the author

mzalendoeditor