Featured Kitaifa

WAZIRI MASAUNI:TENDO LA NDOA SIO HAKI YA MSINGI

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema serikali haiwezi kuruhusu wafungwa kupata  fursa ya kuonana na wapenzi wao kwa ajili ya kufanya tendo la faragha (Ndoa)gerezani kwani hiyo ni haki lakini  sio haki ya msingi .

Mhandisi Masauni amebainisha hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu  swali la mbunge aliyehoji  serikali ina mpango gani wa kuruhusu wafungwa wanapata wasaa wa kufanya tendo la ndoa na wenza wao ili kuondoa upweke.

Katika majibu yake Mhandisi Masauni amesema katika tamaduni za kitanzania na Afrika kwa ujumla  hazijazoea kuona mtu anapotaka kufanya tendo la ndoa na watu wengine wajue kwani hilo ni tendo la faragha.

Hivyo ,Mhadisi Masauni amebainisha kuwa kuna haki za msingi zinazoweza kuzingatiwa kwa mfungwa ikiwemo haki ya malazi,chakula na si tendo la ndoa.

“Kwa utamaduni wetu si vyema kila mtu ajue kuwa fulani anakwenda kufanya tendo la ndoa kwani tendo hilo ni la faragha hivyo,haki za msingi kwa wafungwa ni ,malazi na chakula  na si haki ya tendo la ndoa akiwa gerezani”amesema.

About the author

mzalendoeditor