Featured Kimataifa

PROF.MAKUBI:TANZANIA KUNUFAIKA NA MASUALA YA UGUNDUZI WA VIMELEA VYA MAGONJWA

Written by mzalendoeditor
Picha ya pamoja ya Katibu mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi na uongozi wa wa Maabara ya Afya ya Jamii na Mazingira  iliyopo South Carolina,Columbia

…………………………………………..

 

Na. WAF-South Carolina,Columbia

Tanzania inatarajia kunufaika kwa kupata fursa ya kuwa na ushirikiano katika masuala ya ugunduzi wa vimelea vya magonjwa mbalimbali yanayoathiri nchi yetu pamoja na chemikali zenye athari kwa afya za watanzania.

Hayo yamebainishwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi mara baada ya kutembelea Maabara ya Afya ya Jamii na Mazingira iliyopo South Carolina,Columbia.

Katibu Mkuu huyo ambaye yupo ziara ya kikazi nchini Marekani katika ziara hiyo pia  amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Maabara ya Afya ya Jamii ya South Carolina, Dkt. Nicholas Epie na baadaye kukutana na Mkurugenzi wa Idara ya Afya na Udhibiti wa Mazingira ya South Carolina Dkt. Edward Simmer, pamoja na timu ya uongozi katika taasisi hiyo.

Mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na uimarishaji wa Maabara ya Afya ya Jamii na Mazingira katika Ufuatiliaji wa Magonjwa (survaillence), mbinu za kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na ujenzi wa maabara mpya ya Afya ya Jamii kulingana na mahitaji ya sasa na ya baadaye.

“Kwa kushiriki ziara hii, Tanzania itajifunza kutoka kwa wataalam wa Maabara ya Afya ya Jamii ya South Carolina kwa kuonesha jinsi tunavyoweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo ufuatiliaji wake unahitaji utambuzi wa maabara na mifumo thabiti” amesema Prof. Makubi

Aidha, ameongeza kuwa fursa nyingine itakayopatikana ni ya  kujenga uwezo wa wataalam kwenye wa Tanzania katika masuala ya maendeleo ya kitaaluma na kutumia uzoefu wa nchi ya Marekani katika utayari wa kukabiliana na matukio yanayoathiri afya ya binadamu.

Katika ziara hiyo Prof. Makubi ameambatana na wataalamu wa wizara wakiwemo wa  Maabara ya Afya ya Jamii.

About the author

mzalendoeditor