Featured Kitaifa

DC SHEKIMWERI AISHAURI TAKUKURU KUANDAA VIKAO KAZI NA SEMINA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin_DODOMA

TAASISI ya kuzuia na Kuapambana na rushwa nchini (TAKUKURU) imeshauriwa kuwa na vikao kazi na kutoa  semina ili kuwajengea uelewa watumishi wa Umma.

Hayo yamesema leo Septemba 12,2022 na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri  alipotembelea Mabanda mbalimbali kwenye wiki ya maonesho ya maadhimisho ya Miaka 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utaswala bora yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete ikiwa na na kaulimbiu isemayo “Miaka 20 ya kuhamasisha ulinzi wa hifadhi ya Haki za binadamu na misingi ya utawala bora” ambapo
taasisi mbalimbali za Msaada wa sheria zimeshiriki Jijini Dodoma.

“Lazima tukiri kwamba kuna changamoto kwenye sehemu ya rushwa , vitu viwili naendelea kusisitiza cha kwanza kumlea samaki akiwa mchanga, wanafanya kazi nzuri na mimi kwenye wilaya nimeandaa midahalo tunashindanisha shule kwenye kupinga masuala ya rushwa kwa njia ya mdahalo,
tunawakutanisha wanafunzi wanaofanya midahalo tunawajenga wakiwa wadogo ili wanapokuwa wajue Nchi yao inatakiwa kuwaje”amesema Shekimweri

Aidha Shekimweri amewataka wananchi kujitokeza kwenda kupata elimu juu ya haki mbalimbali ambazo zinatolewa katika viwanja vya Jakaya Kikwete.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora,Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa kama Tume wamekuwa wakipokea malalamiko mbalimbali yakiwemo ya migogoro ya Ardhi,Jeshi la polisi kulalamikiwa kubambikiza kesi pamoja na kutesa wananchi ikiwemo na masuala ya rushwa.

“Nyakati hizi naona malalamiko ya migogoro ya ardhi yanayoletwa si mengi sana lakini yale machache yanayotufikia tumeyashughulikia kwa kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo kwa taasisi husika nakuyachukulia hatua,
Kuhusu masuala ya unyanyasaji haya mara nyingi yakija kwetu kule polisi kuna dawati,tunayapeleka dawati la jinsia na wao wenzetu wanaanzisha mchakato wa upepelezi” amesema Jaji Mwaimu

Maadhimisho hayo yanaenda sambamba

About the author

mzalendoeditor