Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YAAGIZA JENGO LA UFUNDI TOWER  KUANZA KUTUMIKA ILI KUONDOKANA NA MSONGAMANI

Written by mzalendoeditor
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii Stanslaus Nyongo akiongea na waandishi wa habari wakati walipotembelea  jengo la Ufundi Tower katika chuo Cha Ufundi Arusha.
……………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii imeagiza chuo cha ufundi Arusha (ATC) kuanza kutumika kwa jengo la ufundi Tower pindi chuo kitakapofunguliwa ili kupunguza adha ya  mrundikano wa wanafunzi katika madarasa na maabara.
Akizungumza katika  ziara ya kukagua jengo hilo mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki alisema kuwa wameridhishwa na  jengo hilo ambapo limefikia hatua ya  kuweka samani ni vyema wakahakikisha linakamilika ili wanafunzi watakapofungua waanze kulitumia hivyo wahakikishe zoezi hilo linakamilika ili wanafunzi wanapofungua chuo oktoba, 2022 waweze kulitumia.
“Tumefika katika eneo hili na timejionea wenyewe ambapo kuna fedha zilitengwa awali zaidi ya bilioni 3.6 na nyingine tukapitisha wenyewe bungeni  ambazo ni fedha za mkopo wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 na hapa zilikuja bilioni 1.7 kwaajili ya umaliziaji wa jengo hili na tumeona fedha hizo zimefanya kazi vizuri,”alisema Nyongo.
Aidha alisema chuo kitakapofunguliwa jengo hilo lianze kutumika haraka iwezekanavyo lengo likiwa ni kupunguza mrundikano wa ratiba kwa wanafunzi na watumishi.
 kwakweli tumeridhika jengo ni zuri ma tunatoa maelekezo lianze kutumika mapema ili kusudi vijana wanapoingia katika muhula mpya wa masomo waweze kujifunzia hapa,” alisema Nyongo.
“Tunaipongeza sana wizara ya Elimu na uongozi wa chuo cha ATC kwa kazi mzuri ya usimamizi wa hizi fedha na tumeona kabisa kama alivyosema Rais, fedha hizi sio za kuliwa hovyo na kuibwa, kwa hapa tulipofikia tumeona imetumika sawa sawa ujenzi umekwenda vizuri kilichobaki ni kuweka thamani ili lianze kutumika,” Alisisitiza.
Alisema kuwa kama kamati na wabunge watakuwa bega kwa bega kusimamia na kutoa ushauri kwa serikali lakini maeneo ambayo wanaona serilali imefanya vizuri hawataacha kupongeza hivyo kila mtaalamu aliyeaminiwa na kupewa kusimamia miradi ni vema wakawa waaminifu.
kwa upandee wake msimamizi mshauri wa chuo hicho Said Issa alisema kuwa  walipatiwa kiasi sh. bilioni 1.7 kutoka serikalini kupitia fedha za UVIKO-19 kwaajili ya umaliziaji wa jengo la madarasa, maabara na ofisi lililokuwa limefikia asilimia 58.4 ya utekelezaji wake.
Aidha alifafanua kuwa mpaka sasa jengo hilo limefikia asilimia 99 ambapo fefha zilizotumika ni bilioni 1.69 huku wizara ikiwa imetoa sh. milioni 481 kwaajili ya uwekaji wa thamani na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa septemba,2022.
Alisema mradi huo una jumla ya madarasa nane yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 880 kwa wakati mmoja,maabara sita yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 270 pamoja na ofisi 26 zenye uwezo wa kuchukua watumishi 104 ambapo itaisaidia msongamano.
“Kwa ujumla litakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1025 na kuweza kupunguza msongamano wa wanafunzi na watumishi katika madarasa na ofisi lakini pia kupunguza mrundikano wa ratiba za masomo kutokana na uchache wa madarasa na maabara,”alisema Said.
Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakigua jengo la Ufundi Tower katika chuo Cha Ufundi Arusha.
Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha Dkt Musa Chaha(katikati) akielezea jambo kwa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za maendeleo ya kijamii wakati walipokuwa wakikagua jengo la Ufundi Tower katika chuo hicho.
Msimamizi mshauri  wa chuo cha Ufundi Arusha Said Issa akielezea jambo kwa kamati ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii walipotembelea jengo la Ufundi Tower katika chuo hicho.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii Stanslaus Nyongo akiongea na waandishi wa habari wakati walipotembelea  jengo la Ufundi Tower katika chuo Cha Ufundi Arusha.
Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea jengo la Ufundi Tower katika chuo Cha Ufundi Arusha.

About the author

mzalendoeditor