Featured Michezo

GEITA GOLD FC YAANZA NA KICHAPO UGENINI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Written by mzalendoeditor

Na Odilo Bolgas-Mzalendo blog

TIMU ya Geita Gold FC imeshindwa kutamba ugenini baada ya kuchapwa bao 1_0 na wenyeji Hilal Al Sahel FC katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Kombe la Shirikisho barani Afrika uliochezwa nchini Sudan.

Shujaa wa Hilal Al Sahel FC ni Mshambuliaji Omer Shamali alifunga bao dakika ya 5 na kuwapeleka  mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao hilo.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Geita wakicheza kwa mashambulizi ya kushtukiza wa wapinzani.

Timu hizo zinatarajia kurudiana Septemba 18 na 19 mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na mshindi wa hapo atakutana na Pyramid ya Misri.

About the author

mzalendoeditor