Featured Kitaifa

KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI ATEMBELEA KIWANDA CHA DZ CARD AFRICA LTD MABIBO

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Jim Yonazi akisaini kitabu Cha wageni mara baada ya kuwasili alipotembelea Kanda maalumu ya Kiuchumi ya Benjamin William Mkapa  Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Jim Yonazi Septemba 09, 2022 ametembelea  Kanda maalumu ya Kiuchumi ya Benjamin William Mkapa  Mabibo Jijini Dar es Salaam.

Dr. Jim Yonaz amekagua na  kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Kiwanda Cha Kutengeneza SMART CARD cha DZ CARD AFRICA LIMITED  kama anavyoonekana Katika picha mbalimbali  akiwa na  maafisa wa Wizara hiyo  alioongozana nao, Uongozi wa EPZA na kiwanda Cha  DZ CARD AFRICA LIMITED.

Akizungunza mara baada ya kukagua kazi za kiwanda hicho Dr. Jim Yonaz ameahidi kutoa ushirikiano zaidi katika kukuza Teknolojia na Uwekezaji nchini kwa Ujumla ili kuendeleza dhamira Njema ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya Kukuza Uchumi wa Nchi na Kuongeza ajira kwa Watanzania.

About the author

mzalendoeditor