Featured Michezo

SIMBA YAPUNGUZWA KASI LIGI KUU YA NBC

Written by mzalendoeditor

Na Bolgas Odilo_Mzalendo blog

VINARA Simba SC wamepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2_2 na KMC mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Moses Phiri dakika ya 2 akifunga bao safi.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko Katika  dakika ya 48 KMC walisawazisha bao kupitia kwa Mshambuliaji wao Matheo Anthony.

KMC waliendelea kulisakama lango la Simba mnamo dakika ya 58 George Makang’a alifunga bao la pili kwa shuti kali baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Simba.

Simba walisubiri hadi dakika za lala salama walisawazisha bao kupitia kwa Habibu Kyombo aliyetokea benchi dakika ya 89.

Kwa Matokeo hayo Simba wanaongoza Ligi hiyo wakiwa na Pointi 7,sawa na Mtibwa Sugar pamoja na Yanga ,Simba akiongoza kwa kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

About the author

mzalendoeditor