Featured Kitaifa

WAZIRI UMMY MWALIMU ATETA NA MTENDAJI MKUU WA GLOBAL FUND

Written by mzalendoeditor

Na Englibert Kayombo – WAF, Dar Es Salaam.

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu leo amefanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Global Fund Bw. Peter Sands kuhusu uboreshaji wa huduma za afya nchini kupitia miradi ya Global Fund inayotekelezwa hapa nchini.

Waziri Ummy ameishukuru Global Fund kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mapambano dhibi ya Ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi, Kifua Kikuu pamoja na Malaria.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha ubora wa huduma hivyo kwa kushirikiana na Global Fund Serikali inatarajia kufikia malengo yake katika mapambano dhidi ya VVU kwa kuwa na afua zilizolenga kuelimisha na kuhamasisha wananchi kutambua mapema hali za afya zao, kuongeza utambuzi wa watu wapya wenye VVU, pamoja na kuzuia maambukizi mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.

Waziri Ummy ameishukuru Global fund kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa afua mbalimbali zinazolenga kukabiliana na magonjwa mengineyo yakiwemo Kifua Kikuu, Malaria UVIKO-19 ikiwa pamoja na uboreshaji wa mifumo ya Sekta ya Afya nchini.

Kwa upande wake Bw. Peter Sands, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Afya nchini na kutoa kipambuele katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu.

Bw. Sand ameahidi ushirikiano zaidi na kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania kufikia malengo ya Kidunia na kukabiliana na maradhi hayo.

About the author

mzalendoeditor