Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA ATETA  NA NAIBU WAZIRI WA VENEZUELA MHE YURI

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda jana tarehe 5 Septemba 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam na kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali ya ushirikiano kwenye elimu, sayansi na teknolojia.

Mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Mkenda alishudhudia utiaji saini ya makubaliano kati ya Tanzania na Venezuela kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, sayansi na teknolojia uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Balozi Liberata Mulamula na Naibu Waziri huyo wa Venezuela Mhe Yuri Pimentel anayeshughulikia maswala ya Afrika.

About the author

mzalendoeditor