MATAJIRI Timu ya Manchester City wametoka nyuma na kuichapa Crystal Palace mabao 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mshambuliaji mpya, Erling Haaland aliyefunga ambao matatu dakika za 62, 70 na 81 baada ya Bernardo Silva kufunga la kwanza dakika ya 53, kufuatia Eagles kutangulia kwa mabao ya John Stone aliyejifunga dakiia ya nne na eJoachim Andersen dakika ya 21.