Featured Michezo

CHELSEA PUNGUFU YAIZAMISHA LEICESTER CITY

Written by mzalendoeditor

LICHA ya kuwa pungufu kuanzia dakika ya 28 timu ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Leicester City Mchezo wa Ligi Kuu ya Engalnd uliopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge jijini London.

Mabao ya Chelsea yamefungwa na  Raheem Sterling dakika ya 47 akimalizia pasi ya Marc Cucurella na 63 akimalizia pasi ya Reece James.
Katika mchezo huo, Chelsea ilicheza pungufu tangu dakika ya 28 baada ya kiungo wake Conor John Gallagher kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Bao la kufutia machozi la Leicester City limefungwa na Harvey Lewis Barnes dakika ya 66 akimalizia pasi ya mkongwe, Jamie Richard Vardy.

About the author

mzalendoeditor