Featured Kitaifa

WADAU WA MAENDELEO NCHINI WATAKIWA KUGUSA JAMII WANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Written by mzalendoeditor

Na. WAF- DODOMA

Wadau wamaendeleo nchini wametakiwa kufanyakazi kwa kuwagusa wananchi ili kuleta ufanisi wanapo tekeleza majukumu yao ili kufikia malengo.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Gwodwin Mollel katika hafla ya kupokea gari kutoka Shirika la Maendeleo ya Watu wa Marekani (USAID) kwa lengo la kusaidia kitengo cha elimu ya afya kwa umma kuifikia jamii katika kuleta uelewa juu ya maswala ya afya nchini

Dkt. Mollel amesema kuwa kuna haja kubwa ya wadau kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuwafikia wananchi na kuhakikisha jamii inasaidiwa katika kutatua changamoto za kiafya katika maeneo yao.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo ya Watu wa Marekani (USAID) Dkt. Ify Udo ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya ambao ndio wenye jukumu la kulinda afya za wananchi na kuhakikisha afya zao ziko salama.

About the author

mzalendoeditor