Featured Kitaifa

UTEUZI: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  • Amemteua Bw. Peter Ilomo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Bw. Ilomo ni Katibu Mkuu Mstaafu. Bw. Ilomo anachuka nafasi ya Dkt. Moses M. Kusiluka ambaye amemaliza kipindi chake.

  • Amemteua Bi. Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Bi. Mahiza ni Skauti Mkuu Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendoeditor