Mratibu wa Sensa Taifa ,Seif Kuchengo ,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa tathmini ya mwenendo wa zoezi la sensa ya watu na makazi.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imetoa tathmini ya mwenendo wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambalo limeanza rasmi Jana nchini kote na tayari wameshawafikia watu milioni10.26 huku ikieleza changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo.
Hayo yamesemwa leo Agosti 24,2022 jijini Dodoma na Mratibu wa Sensa Taifa ,Seif Kuchengo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na zoezi hilo.
Bw.Kuchengo amesema kuwa tathmini imeenda vizuri kutokana na mifumo yao kuweza kupokea taarifa kama walivyo tarajia kwani zoezi hilo na mafanikio yake yyamepimwa kwa siku ya kwanza ambayo ilikuwa ni jana.
”Kwani nchi nyingine za jirani hazikuweza kufanikiwa kutuma data na kupokelewa na hivyo kutoleta maana kazi ilifanyika jana kwa asilimia 15 ikiwa ni asilimia 0,45 zaidi ya malengo yetu tuliyojiwekea”amesema Bw.Kuchenga
Aidha amesema kuwa kwa siku ya kwanza karani aliekuwa anaenda kuhoji watu ni kama alikuwa anajifunza lakini kadri siku zinavyoendelea anazidi kuimarika na kufanya zoezi hilo kwa uharaka zaidi
Hata hivyo ameeleza kuwa leo wanatarajia kuwa na idadi ya watu watakaohoji itakuwa ni kubwa kuliko jana na wameweza kuhoji kaya milion 2.35 sawa na idadi ya watu milioni10.26.
”Makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka huu kutokana na sensa ya watu na makazi iliyopita inakaribia kufikia milioni 61.3 na makadirio hayo yanaweza kuongezeka na kufikia milioni 64.
Mratibu wa Sensa Taifa ,Seif Kuchengo ,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitoa tathmini ya mwenendo wa zoezi la sensa ya watu na makazi.