Featured Kitaifa

RAIS DKT.MWINYI AWEKA ANUWANI YA MAKAZI KATIKA MAKAAZI YAKE MIGOMBANI

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka Nambari ya Anuwani ya Makazi 78 Barabara ya Julius Nyerere katika Makaazi yake Rais wa Zanzibar eneo la Migombani leo 22-8-2022.na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawailiano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka Nambari ya Anuwani ya Makazi 78 Barabara ya Julius Nyerere katika Makaazi yake Rais wa Zanzibar eneo la Migombani leo 22-8-2022.na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawailiano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed, akitowa maelezo ya Anuani ya Makaazi, baada ya uwekaji wa anuani hiyo uliofanyika leo 22-8-2022, katika Makazi ya Rais wa Zanzibar eneo la Migomani Wilaya ya Mjini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.(hawapo pichani) baada ya uwekaji wa Anuwani ya Makazi ya Rais wa Zanzibar eneo la Migombani Wilaya ya Mjini na (kulia kwa Rais ) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor