Featured Kitaifa

MAGU YATAFUTA MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA WAFUGAJI KATIKA HIFADHI YA SAYAKA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Salum Kali amekutana na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya hiyo kujadili mikakati ya kutatua changamoto ya wafugaji katika Hifadhi ya Sayaka Wilaya ya Magu.

Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magu.

Mhe.Kali amesema moja ya mwarobaini wa tatizo hilo ni kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuzuia wananchi kuingiza mifugo hiyo hifadhini.

Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe Mary Masanja amesema suala la uvamizi wa hifadhi ya Sayaka linatakiwa kutatuliwa kwa kushirikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

About the author

mzalendoeditor