Featured Michezo

WADAU WA MICHEZO DODOMA WAILILIA TFF KUFUNGIWA KWA UWANJA WA JAMHURI

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-DODOMA

WADAU wa Michezo Mkoani Dodoma  waeleza hisia zao tangu kufungiwa kwa uwanja wa Jamhuri  ambapo uwanja huo ulibainika na makosa katika sehemu ya kuchezea Pitch yake kutokidhi viwango  na kusababisha kufungiwa na Bodi ya Ligi ya TFF.

Hayo yamesema leo na Meneja wa Uwanja wa Jamhuri Dodoma Anthony Nyambera,wakati akifanya mahojiano na  Mzalendo blog leo Agosti 18,2022 amesema Wamepata malalamiko mengi tangu kufungiwa kwa uwanja lakini tayari uwanja upo sawa na wamesharekebisha makosa yote ambayo yalibainika katika uwanja

“Uwanja wetu umefungiwa tangu tarehe 16 Agosti, 2022 ambapo tumepewa siku 14 za kurekebisha Uwanja na makosa sio kwamba ni makubwa ila ni madogo tu yakurekebeshika”, amesema

“Mpaka sasa uwanja umekaa sawa na tayari kwa mechi zijazo najua wakija wakaguzi watapitisha na mechi sizajo watakuja kucheza hapa nyumbani”.Amesema

Naye Benjamin Songo Mkazi wa Bahi raod amefunguka na kusema tangu uwanja ufungiwe wamepata changamoto nyingi kutokana na Timu nyingi Mkoani Dodoma wanatumia uwanja huo kwaajili ya michezo pamoja na kutazama Timu yao ya Jiji.

“Sisi tulishazoea kutazama mpira hapa, sasa tangu umefungiwa tupo mtaani hatuelewi mechi zetu tutazitazama wapi, tena na sisi wa viwango vya chini hatuwezi kufika mikoani kwaio uwanja huu kwetu sisi unatusaidia kutazama hapa karibu”, amesema

“Kama Jana timu yetu ilitakiwa kuchezwa hapa Jamhuri sasa kutokana na Kufungiwa kwa Uwanja wameamua kwenda kucheza singida kwakweli tumejisikia vibaya”.Amsema Songo

Abogasti Munishi Mkazi wa Dodoma ameongezea kwa kusema wamepata pigo hasa na kusababisha timu ya Jiji kutocheza uwanjani na kupelekea kupoteza mchezo wake jana Mkoani Singida.

“Sisi tuliamini tunashinda lakini ikawa tofauti kama tulivyopanga na kusababisha kupoteza mchezo na timu yetu kama ingecheza nyumbani ingekuwa tofauti na tungepata ushindi

kutokana na mashabiki wengi wangekuwepo kusapoti timu na pia wangekuwa huru na uwanja wao” .Amesema Munishi

About the author

mzalendoeditor