NAIBU Waziri wa Maji MarryPrisca Mahundi akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayani Handeni ikiwemo kutembelea tenki lenye uwezo wa kuhifadhia maji lita 167,000 unaotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha wananchi waliohamia kutoka wilaya ya Ngorongoro wanapata huduma ya maji safi na salama.
MKUU wa wilaya ya Handeni Siriel Mchemba akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Na Oscar Assenga,
NAIBU Waziri wa Maji Marry Prisca Mahundi ametoa siku saba kwa
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Handeni Mhandisi Hosea Joseph kuhakikisha anamsimamia
mkandarasi wa Kampuni ya Mponela Dicksona Mwipoo anayetekeleza mradi wa maji
katika Kijiji cha Msomera wilayani humo kuhakikisha maji yanafika kwenye tenki
na kuyasambaza kwa wananchi.
Agizo la Naibu Waziri huyo alilitoa leo wakati wa ziara yake
ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayani
Handeni ikiwemo kutembelea tenki lenye uwezo wa kuhifadhia maji lita 167,000 unaotekelezwa
na Serikali ili kuhakikisha wananchi waliohamia kutoka wilaya ya Ngorongoro
wanapata huduma ya maji safi na salama.
Alisema kwamba thamani ya hilo tenki ni kuhakikisha linatoa
maji na yapelekwa kwa wananchi waliopo kwenye Kijiji hicho ili kuweza
kuwaondolea changamoto ambazo wanakumbana nazo kusaka huduma hiyo muhimu kwa
maendeleo yao na jamii zinazowazunguka.
Aidha alisema wao kama Wizara ya Maji mahali popote wanapoona
wananchi wanakwenda kujenga kuishi wanahitajika kupatiwa huduma ya maji na kwa
hapo Msomera maji yalikuwa yanapatikana kwa wingi kwa jitihada ambazo zimefanywa
na Tanga Uwasa na Ruwasa.
“Niwapongeze Ruwasa ambao wanasimamiwa na Mhandisi Upendo Omari
ambaye anafanya kazi nzuri sana hapa tulipo kuna tenki kubwa ambalo lililetwa
kutoka nje lengo kuhakikkisha jamii ya msomera inapata maji toshelevu na kwa
kupata tenki hili visima vilivyochimbwa hapa vinakwenda kutumika vizuri”Alisema
Naibu Waziri huyo alisema kuna kisima ambacho kinatoa maji
mengi na wanategemea ndani ya wiki moja kutoka leo hiikitaanza kusafirisha maji
kutoka eneo hilo na kwenda kwenye tenki na baadae usambazaji wa maji kwa wananchi wataohamia hapa Msomera wanapata
huduma ya maji.
“Niwahakikishie kama Serikali kupitia Wizara ya Maji muwe na
uhakika mtapata maji kwa matumizi ya majumbani ya uhakika na jamii ina mifugo
kwa sababu ya hilo tumejenga maeneo ya kunyeshea mifugo msomera matatu ili
kuhakikisha wanyama wanapata maji ya kutosha na tunatambua kenye kundi hili
kuna wakulima tayari waziei wa Kilimo atakuja lengo la kuhakikisha pia tunapata
wakulima kupitia kilimo cha Umwagiliaji”Alisema Naibu Waziri huyo.
Alisma kwa sababu unjengeji wa nyumba unendelea katika eneo
hilo watendelea usambaji wa maji na wanancji wanaendelei kupata maji karibu kwa
sababu ujengeji nyuma unaendeleo kusambaa wengine watajikuta wanakuwa mbali na
vichoeta maji vyao watawafuata walipo lengo
kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi kwa wananchi.
Hata hivyo alisema kwamba maji yakishafika kwenye tenki
yatakwenda kwenye usambazaji wa vichotea maji na kwa wananchi watakaokuwa na
uhitaji wa kuyavuta kwenye majumba yao watapewa vigezo vya na masharti nafuu
ili waweze kuvuta maji,
“Lakini nitoe wito kwa wakandarsi wote ambao mnapewa kazi nchi
mhakikisha mnafanya kazi kwa kujituma bila kuangali malipo yamelipwa kwa wakati
au yamechelewa huyu mkandarsi hapa amefanya kazi nzuri tutaendelea kufanya naye
kazi Wizara ya maji ipo chini ya Waziri Jumaa Aweso na Rais Samia Suluhu imedhamiria
kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani ili waweze kufanya shughuli nyengine za
kuchangia kwenye pato la Taifa kwa kufanya shughuli za uzalishaji “Alisema
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja wa Ruwasa Mkoa
wa Tanga Mhandisi Upendo Omari alimueleza Naibu Waziri huyo kwamba wamepokea maelekezo
hayo na wao watahakikisha kwamba ndani ya siku tatu wananchi wa eneo hilo wanapata
maji.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel
Mchemba alisema kuwa kabla ya kuingia Serikali ya awamu ya sita hali ya
upatikanaji wa maji ili kuwa chini ya asilimia 34 ambapo ndani ya kipindi cha
mwaka mmoja hali ya upatikanaji wa maji umefikia asilimia zaidi ya asilimia 50.
Aidha alisema Wilaya hiyo imefanikiwa kupata zaidi ya Bil 10
ambapo bil 1 inatokana na fedha zitokanazo na uvico ambzo kwa ajili ya Handeni
Mjini na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya kuondoa tatizo la maji
ambalo lilikuwa linaikumba Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Handeni Hosea
Joseph alimuhakikishia Naibu Waziri wa Maji kuwa amepokea agizo la kumsimamia
Mkandarasi Mponela Construction and co,ltd anaetekeleza ujenzi wa mradi wa maji
Kijijini hapo kuwa utamalizika kwa
wakati kama agizo lilivyotolewa.
Hata hivyo alisema mbali ya agizo hilo la siku saba
alisisitiza kutokana na umuhimu wa huduma hiyo ya maji atahakikisha ndani ya
siku tatu wananchi wa kijiji hicho watakuwa wanapata huduma hiyo ya maji ili
kuondoa kero iliyopo ndani ya makazi hayo ya wananchi waliohamia katika eneo
hilo.