Featured Kitaifa

BARRICK ILIVYOSHIRIKI UZINDUZI WA KIPINDI CHA THAMANI YA MADINI

Written by mzalendoeditor
Kampuni ya Madini ya Barrick, imeshiriki na kudhamini mbio za Madini Marathon zilizofanyika mjini Shinyanga ambazo zilienda sambamba na uzinduzi wa kipindi kinachohusu sekta ya madini kinachojulikana kama Thamani ya madini kitakachorushwa na kituo cha Runinga cha Channel Ten ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko.
Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko akizungumza Agosti 14,2022 wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Thamani Madini kitakachokuwa kinarushwa Channel Ten
Kaimu Meneja Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akiongea kwa niaba ya kampuni katika hafla hiyo.
Kaimu Meneja Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akiongea kwa niaba ya kampuni katika hafla hiyo.
Msimamizi wa ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Michael Mhanuka Wilson akiongea wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Thamani Madini kitakachokuwa kinarushwa Channel Ten
Wafanyakazi wa Barrick wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Barrick walishiriki kupiga picha ya pamoja na mgeni rasmi,Waziri wa Madini,Dk.Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Sophia Mjema.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick wakifuatilia matukio ya michezo ya Madini Marathon

About the author

mzalendoeditor