Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA MKOANI TANGA ATAZINDUA CHUO CHA JESHI LA UHAMIAJI

Written by mzalendoeditor

Na Oscar Assenga,TANGA.

RAIS
Samia Suluhu anatarajiwa kuwasili kesho mkoani Tanga kwa ajili ya ziara
ya siku mbili mkoani Tanga ambapo akiwa mkoani hapa  atazindua Chuo cha
Jeshi la Uhamiaji cha Taifa.

Akizungumza leo wakati wa halfa ya
kukabidhiwa ofisi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema Rais Samia
ataingia mkoani Tanga kesho mchana na Jumatatu  atafanya ziara wilayani Mkinga

Mgumba
alisema Rais Samia atazindua chuo hicho cha Jeshi la Uhamiaji
kilichojengwa eneo la Boma KichakaMiba wilayani Mkinga ikiwemo kufunga
mafunzo ya wanajeshi wa jeshi jipya la Uhamiaji zaidi ya 818 waliohitimu
mafunzo.

Alisema baada ya Rais Samia ataondoka ambapo pia alitoa
rai kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumlaki katika maeneo
yote atayopita.

About the author

mzalendoeditor